ANGALIZO KWA MABINTI

ANGALIZO KWA MABINTI, USIPUUZE..!!
Mimi sikukatazi kutumia mwili wako kama kitega uchumi.
Sikukatazi kulala na wanaume kwaajili ya pesa,mavazi,vipodoxi na hata magari
Lala na kila mwanaume unayemwona mbele yako.
Endelea tu  kubadili wanaume kama hereni leo unavaa nyekundu kesho pinki.
Endelea kuweka rekodi ya kulala kwenye mahotel mengi na wanaume tofauti tofauti.....Oriental hotel, sheraton hotel n.k
Endelea kuwapanga tu mpaka idadi ya wanaume uliolala nao iwe kubwa kuliko hata umri wako mfano una miaka 25 na umeshalala na wanaume 30 tofauti tofauti.
.
.
Endelea tu kuwa mama huruma mtaani na kuwachuna wanaume kwasababu tu unataka kwenda na wakati:
Unataka kutumia simu ya kisasa:
Unataka kuseti nywele za bei kubwa.
Unataka kuvaa nguo za bei ghali, na Kutembelea magari.
we wachune tu.
Na zile kauri zako za dharau pia usiziache "Its
none of ur business"
Ni kweli hainihusu na wala sina mpango na hayo unayofanya.
.
.
Ila utakapoanza kuona inanihusu ni pale utakapoanza kufungua mdomo wako na kusema unatamani mwanaume wa kukuoao akupende hivo hivo ulivyo
Hususani pale utakapokuwa umri wako umeenda na umeshapoteza kila kitu hujabakiwa na chochote cha kusema utaringia
Hapa ndo utaanza kutamani mwanaume yeyote akutongoze uende ukakatalie geto ili tu upate kuolewa.
Pamoja na yote kuolewa ndo utaolewa ila Mungu lazima atakupa mwanaume wa kuendana na ww mwanaume ambaye nae atakuwa alishafanya matukio ya ajabu na yasiyo simulika siku zake za nyuma
Na huyo ndo atakuwa mume wako.
.
.
Baada ya miaka miwili tu ya ndoa yako utakuwa unaanza sasa kujipashapasha kwa kwenda makanisani maana yawezekana ulishapoteza kizazi chako katika harakati za kutoa mimba mfululizo ili tu kuendelea kuufaidi ujana.
Wakati huu ndo utakapoanza kuwatafuta wachungaji na kuhamahama makanisa leo kwa mchungaji huyu kesho kwa yule mara leo kanisa hili kesho lile
Lengo tu kuutafuta muujiza uweze kupata mtoto.
Unasahau kuwa ulishatoa mimba nyingi na ulishatupa watoto kibao.
Utalia sana na kutamani nikuonee huruma
Lakini mm nasema kama ni kulia we lia tu hata machozi ya damu.
Mm ninaowaonea huruma na kuwasikitikia ni wale ambao hawajapata watoto kwa mpango wa mungu na sio wanaojitakia kama ww Ebooo
Nategemea hapa wakunichukia watakuwepo maana ukweli unauma.
Nimeeleweka??


ANGALIZO KWA MABINTI ANGALIZO KWA MABINTI Reviewed by Unknown on December 29, 2017 Rating: 5

1 comment:

Powered by Blogger.