DHAMBI YA KUANGALIA PICHA ZA NGONO

Picha za uchi na za ngono hazikutengenezwa kwa lengo la kukupatia burudani wala kukupatia furaha; zilikusudiwa kwa lengo la kuwaangamiza kabisa watengenezaji na watazamaji wake. Humjaza mtu husika hashiki na tamaa kali ya kimapezi na humfanya aendelee kutaka kuangalia zaidi na zaidi. Matokeo yake ni kwamba huibuka ndani yake vitendo viovu sana na ukatili wa kimapenzi, huelekea katika njia ya uangamivu wa  hakika kwa sababu ya kushindwa huku kujitawala.

Watu wasio na akili hupenda kutazama picha na video hizi bila kujua kuwa wanaalika mapepo ya tamaa ya mwili ndani yao wenyewe. Ni njia kuu kabisa ya kualika mapepo katika maisha ya mtu. Wala mapepo hawahitaji kuwa na funguo za ziada kuingia ndani yako. Wanachohitaji tu kufanya ni kukushawishi uangalie picha zao chafu hata kama ni kwa kiasi kidogo tu, na hapo ndipo tayari umekuwa umewaalika katika maisha yako! Utaendelea zaidi na zaidi, na kwa wengi huwa jambo la kawaida; japo utatamani kujinasua, lakini hutakuwa na nguvu hizo kwa sababu ya kushikiliwa na nguvu za giza! Unapokaa mwenyewe kuangalia picha hizi, hauko peke yako!

Huwa umezungukwa na malaika waovu wakitazama udhaifu wako ili waendelee kukushambulia na kukushinikiza zaidi na hatimaye kukuangamiza kabisa. Wanapogundua udhaifu wako katika eneo ili, hapo ndipo huendelea kukushambulia na kufanya iwe ngumu sana kwako kushinda. Ndiyo maana watu ambao wanajihusisha katika vitendo hivi, hata ingawa hufanya maamuzi ya mara kwa mara kuacha na kujiepusha nayo, hujikuta tu wamerudia dhambi ileile tena na tena!

Lakini habari njema ni kwamba, bado unaweza kushinda na kuutawala mwili wako vyema kwa uwezo wa Mungu! Anasema, “Mtiini Mungu; mpingeni Shetani, naye atawakimbia.” Kwa njia ya kumtegemea Yeye na kuwa na nidhamu ya maisha yako, kwa njia ya kufunga na kuomba, unaweza kuwa mshindi kabisa. Vinginevyo, mapepo hayo ya kishetani yatakuteka kabisa na kuwa kikwazo katika njia yako ili kukunasa, na kwa kweli utakuwa ukipuuzia mambo ya msingi ya kimaisha, na kila wakati utapenda kupoteza muda na rafiki wasiojali ili kuendekeza tamaa za mwili. Ndio maana maisha ya watu wengi, hasa vijana, pamoja na kuwa wana uwezo mkubwa sana wa kiakili, wana fedha, lakini maisha yao hayana maana—wanaishi bila kuridhika na wanatumikia mwili wao kwa ubinafsi, hadi wanapofikwa na mauti ya ghafla bila wao kujua, na huo ndio mwisho wa maisha yao! Wamepoteza nguvu, akili na ubora na manufaa yao wakati ambapo wangeweza kuwa watu wanaoheshimika na wenye kuleta faida na maendeleo bora katika jamii na taifa.

Tunapaswa kutambua kuwa waigizaji na wale wanaojihusisha kuangalia picha na video za ngono hutumiwa na mashetani ili kujihusisha katika uovu na ufuska mkubwa sana uliopita kiasi huku wakidhalilisha na kufedhehesha miili yao. Wanaume waliooa ambao wametekwa na uraibu wa ponografia hujikuta kwamba ni vigumu sana kufanya mapenzi bora na wake zao, na kuridhika; vijana ambao hawajao pia hujihusisha katika vitendo vingine viovu zaidi kama vile kupiga punyeto, nk.

Ni dhahiri kwamba madhara ya picha za ngono ni makubwa sana. Channel za televisheni, mitandao, magazeti na kadhalika, vinavyohusika na vitu hivi vina lengo moja tu la kuharibu kabisa maisha yako, na hatimaye kukuangamiza bila wewe kufahamu. Sehemu ya kubwa ya uovu duniani hutokana na kujihusisha na vitendo hivi. Ni hatari vilevile kuangalia picha na mikanda au video za ngono hata kama umeoa au hata kama uko na mkeo. Mungu kamwe hawezi kuruhusu machukizo hayo ya kishetani kwa sababu anajua huangamiza moja kwa moja uhusiano bora wa kimapenzi kati yenu, huvuruga akili na kuharibu na kuangamiza maisha yako bila wewe kujua. Hukufanya uwaone jinsi ya kike kama vyombo vya ngono! Na mbaya zaidi, ni dhambi kuu dhidi Yake.

Kwa hiyo wapendwa hebu fanya uamuzi wa dhati tangu sana kwamba unahitaji kukombolewa kutoka katika picha na video za ngono, wakati huu ambapo bado ungali na nafasi ya kutubu na kufanya mabadiliko, kabla maisha yako hayajaangamizwa. Baadhi ya watu huthubutu kuingiza picha chafu hata kwenye mitandao ya kijamii. Usifungue video hizi! Kwenye mtandao wa WhatsApp zima settings za autodownload ili picha au video zikiingia zisiweze kupakuliwa moja kwa moja. Mtahadharishe mhusika juu ya madhara yake. Wabloku watu wa namna hiyo kwa sababu hawakutakii mema na wanakupeleka jehanamu! Waonye vijana na wapendwa wanaoelekea katika hatari hii bila kujua. Jihusishe katika mambo mema yanayojenga akili na kuleta tija katika maisha yako.

Maneno Ya Mungu yanatuambia:

“Wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi; bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki.” Warumi 6:13.

*TAFADHALI SHARE UJUMBE HUU KWA WATU WENGI NA MARA NYINGI KADIRI IWEZEKANAVYO ILI KUOKOA MAISHA NA ROHO ZA VIJANA WENZETU WAPENDWA!!!*

DHAMBI YA KUANGALIA PICHA ZA NGONO DHAMBI YA KUANGALIA PICHA ZA NGONO Reviewed by Unknown on January 01, 2018 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.