KWANINI TUNAINGIA KWENYE NDOA NA WATU WASIO SAHIHI


•Sex; Ndio sex, yaani Ngono; Sex inapokua mapema ni kama kulisha kuku wa kisasa. Inafanya mahusiano yakue haraka bila kuwa na uimara au ubora wenye virutubisho vyenye ladha.

Sex ya mapema inatengeneza kitu kwa kitaalamu kinaitwa GMR - Genetically Modified, Relationship au Early maturing. Badala ya kifikiria jinsi ya kufanya mahusiano yawe bora, mtaanza kufikiri namna ya kufanya sex vizuri zaidi mtakapokutana next time.

Badala ya kutizama kama partner wako anafaa kuwa mume au mke, utaanza kutizama kama partner wako yuko vizuri au vibaya kitandani. Badala ya kupanga pamoja future yenu, mtakua mkipanga pamoja style za sex basi, kama vile mnajiandaa kutengeneza video za ngono.

• Money (Pesa):  Ndio maana maandiko yanasema pesa ndio shina la kila mabaya (1 Timothy 6:10)...pesa zinaweza zikakufanya uoe au uolewe na mtu asie sahihi.

Mathalani, mwanaume anapokua na pesa, wanawake wapenda pesa tu wataanza kujitokeza na kujigonga kwake, itaongeza chances za yeye kuoa wale wanaopenda pesa zake tu. Pesa zitampiga upofu na wala asione mtu sahihi.

Vivyo hivyo, hata mwanamke anapokua na pesa, wanaume bora wasio jiamini watamuogopa, watajenga picha ya mwanamke alie na kiburi kutokana na pesa zake..hivyo basi huyo mwanamke atawavutia zaidi ma-handsome wenye pesa zaidi ambao hawana la ku-offer zaidi ya "Vitamin-D".

Kuwa na pesa nako ni kikwazo kikubwa katika kupata mtu sahihi. Busara na mtizamo ulio chanya vinahitajika sana.

•Good looks (Muonekano mzuri): Ushawahi kuona reaction ya wale wanawake wanaojiona wazuri ukiwafuata. Kwa sababu wanajiona wako na demand kubwa, huwakataa wanaume walio bora na wanaongeza bar of standards.

Kwa kufanya hivyo wanawakosa kabisa wale wanaume walio na nia ya dhati. Vilevile, katika kutafuta life partner, uzuri umekua ni giza linalofunika mengine mazuri ya mtu husika yasionekane. Bila ya kufahamu kuwa hata shetani (Lucifer) nae alikuwa ni mzuri mno na aliyeng'aa kabla ya kutaka kujiinua na Mungu akampiga chini.

Usikubali hips zikudanganye, usiruhusu six pack zikupige upofu...kwenye ndoa kuna zaidi ya muonekano wa nje wa mtu. Sasa oa/olewa na uzuri wa mtu uone kama huo uzuri utaleta thamani yoyote kwenye hiyo ndoa.

My wisdom,Ndoa njema sio pale wapenzi  wakamilifu wanapo oana bali ni pale wapenzi wasio kamili wanajifunza kuvumiliana na kufurahia tofauti zao "
"A great marriage is not when the ‘perfect couple’ comes together. It is when an imperfect couple learns to enjoy their differences."

A word is enough for the wise....!


KWANINI TUNAINGIA KWENYE NDOA NA WATU WASIO SAHIHI KWANINI TUNAINGIA KWENYE NDOA NA WATU WASIO SAHIHI Reviewed by Unknown on January 01, 2018 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.