NITAMWAMBIAJE KWAMBA NAMPENDA

Mmoja wa marafiki zangu aliwahi kuniuliza "nitamwambiaje mwanamke kwamba nina mpenda na ninahitaji kuwa na yeye" Swali hili ni miongoni mwa maswali ambayo hupita katika akili ya kila binadamu mwenye hisia na jukumu la kutaka kuwa na mwanamke au mwanaume ampendaye. Ni ukweli ulio dhahiri kuwa sote tunahisia na kunawatu tunawapenda na tunatamani wawe katika maisha yetu kama wapenzi. Lakini swali la msingi ni kwa jinsi gani tunawaambia hawa watu hisia zetu? Mara nyingi huwa mtu unajikuta unafikiria sana, labda nikimwambia kwamba ninampenda itakuwa mapema sana ukizingaria ndio kwanza nimekutana nae mapema wiki hii. Mara nyingi hofu hutanda ndani ya moyo kila mara unapofikiria ni kwa jinsi gani utamwambia kwamba unampenda. Kabla ya kumwambia mtu kwamba unampenda ni vyema ukajaribu kuchunguza mambo yafuatayo ili kuona kama mtu huyo anaonyesha kuvutiwa na wewe au lah,

1. Je huwasiliana na wewe mara kwa mara? hapa angalia namna anavyokujibu kila mara ukimtafuta? Je niwewe ambaye umekuwa ukimtafuta kila wakati lakini yeye huwa hakutafuti? Kama huwa anawasiliana na wewe mara nyingi basi nafasi yako ya kuwa naye ni kubwa.

2. Je huzungumza habari zako kwa ndugu na marafiki zake? Kama huwa anakuzungumzia mbele ya rafiki na ndugu zake basi ni mtu ambaye anajivunia kuwa na wewe. Nafasi yako ni kubwa

3. Je hukununulia zawadi?

4. Je hukushika mkono pindi mtembeapo pamoja?

5. Je hukwambia kwamba anafurahi kuwa na wewe?

6. Je kwa namna gani huwa anakutazama? Lugha ya macho ni muhimu sana. Macho ya binadamu huzungumza kwa namna nyingi hata kipindi mdomo ukiwa umefungwa, hivyo namna anavyo kutizama inamater.

7.Je huzungumza habari za mwanaume au mwanamke mwingine pindi muwapo pamoja?

8. Je huzungumzia nia ya kutaka kuwa na wewe kwa miaka ijayo?

Jaribu kuchunguza mambo hayo kabla ya kumtamkia kwamba wampenda. Sio lazima yote yaonyeshe kukubali lakini nusu ya mambo hayo ni dhahiri kwamba hauko mbali sana katika fikira zake. Ukisha kujiridhisha jiamini mchukue uende nae sehemu tulivu mzungumze kwa utulivu.

Hakuna sababu ya kuwa na papara katika hili maana siku ya kwanza huwa inamaana kubwa sana. Kama ukivuruga hapa basi ni vigumu kumpata mtu umpendae kabisa. Fanya kwa utulivu waweza shika mkono wake na kumwambia kwa utulivu "NAKUPENDA NAHITAJI KUWA NA WEWE". Mara nyingi hii ndio sentensi iliyo ngumu kutamka ukiisha kusema haya subiri uone atazungumza nini 

UTAFANYA NINI ASIPO SEMA ANAKUPENDA PIA 
Hakuna haja ya kupaniki wala kukosa amani kama asipokujibu kwa wakati huo huo kwamba anakupenda pia. Haina maana kwamba hakupendi ila inawezekana hakutegemea kusikia kitu kama hicho toka kwako. Kuwa huru unaweza kubadilisha mada na kuzungumzia jambo jingine, hakuna haja ya kuendelea kurudia rudia kila wakati kwani unaweza kumfanya akaacha kuvutiwa na wewe.

USIMLAZIMISHE 
kama hajasema anakupenda pia hakuna sababu ya kumlazimisha jaribu kuwa na subira. usiweke nguvu nyingi kutaka akupe jawabu ndani ya siku moja, kuwa mpole na siku zote kuwa karibu nae mpaka pale atakapo kwambia kwamba anakupenda au hakupendi. Na siku zote jawabu la mwanzo atakalo kupatia hilo ndio jawabu sahihi. 

MUHIMU 
Huna uchawi wala kanuni ya kumfanya mtu akupende. Kama kungekuwa na kanuni maalumu basi mapenzi yengekuwa hayana THAMANI yoyote Usite kuacha maoni yako kwenye kisanduku cha maoni hapo chini. Na pia kutembelea ukurasa wetu mara nyingi kupata mada mbalimbali kuhusu maisha na mahusiano



NITAMWAMBIAJE KWAMBA NAMPENDA NITAMWAMBIAJE KWAMBA NAMPENDA Reviewed by Unknown on January 05, 2018 Rating: 5

2 comments:

Powered by Blogger.