KWANINI MPENZI HUBADILIKA BAADA YA NDOA JE KUNA NAMNA YA KUMZUIA ASIBADILIKE

KWANINI HUYO MCHUMBA/MPENZI WAKO ATAKUJA KUBADILIKA BAADA YA NDOA, JE, UNAWEZA KUZUIA ASIBADILIKE?

Kila siku nilikua nikiulizwa maswali haya, “Mume wangu kabadilika baada ya kunioa nifanyeje? Amenioa kaanza dharau? Nimemuoa kabadilika sana? Mume wangu kawa mtu wa pombe zamani hakua hivyo? Mume wangu amekua mchoyo, hajali tena hisia zangu!” Haya ni maswali ambayo nilikua nikipokea kila siku, Mabadiliko! Mabadiliko! Mabadiliko!

Ingawa maswali mengi yalikua kwa wanawake lakini ilionekana kua karibu kila ndoa mwenza/mwanaume hubadilika baada ya kuoa na kwa bahati mbaya hubadilika kutoka kua mwanaume bora na kuwa mwanaume kichomi, huonyesha tabia ambazo awali alikua hana na hazivumiliki! Hii ilinifanya kujiuliza, hivi ni wanaume wa sasa tu ambao hubadilika?

Je, zamani ilikuaje, mbona ndoa za zamani zilikua zinadumu sana? Je wanawake wa zamani walikua wavumilivu sana kuliko wa sasa au ni nini? Kwasababu hiyo, ili kupata majibu ya maswali yangu niliamua kufanya utafiti, wakati naandika Kitabu changu cha “Ndoa Yangu Furaha Yangu” niliongea na watu (akina Mama) ambao ndoa zao zilikua na zaidi ya miaka 30.

Swali langu lilikua moja je waume zao wamebadilika baada ya ndoa? Karibu wote waliniambia hapana, lakini nilipowauliza kabla ya ndoa walikuaje na baada ya ndoa wakoje karibu wote walikua hawawafahamu waume zao kama wapenzi kwamaana ya kabla ya ndoa. Utasikia mimi walikuja wazee wao kwetu wakaongea na Baba nikaolewa, utasikia ilitumwa posa na tulikutana siku ya harusi.

Kwamba hawakua wakiwafahamu waume zao kabla ya kuoana hivyo tabia walizokutana nazo hawawezi kujua kama wamebadilika au la, hapa nikimaanisha kwamba tofauti na sasa ambapo unajuana na mume au mke wako miaka mitatu kabla ya kuoana zamani hakukua na kujuana kabla. Kwa maana hiyo sio kama wanaume wa zamani au wanawake walikua hawabailiki, hapana nikwakua walikua walikua hawajuani kabla.

Baadaya hapo nilirudi katika kizazi cha sasa na kuangalia ni kitu gani kinatokea. Hapa niligundua kuwa wakati wa uchumba watu wengi huishi kwa kuigiza, si hamuonani kila siku hivyo kila mtu hujaribu kuficha tabia zake mbayambaya zote kwa mwenzake, lakini baada ya ndoa kila mmoja hurelax na kwakua sasa mnaishi nyumba moja, usiku na mchana basi inakua ngumu mtu kuficha tabia zake kila siku.

Labda twende na kitu kimoja, mwanaume ambaye tabia yake ni kurejea usiku,huwezi kuiona kwakua hamuishi pamoja, kwamba hata kama unaenda kwake kulala basi ni siku moja moja. Unapokua unaenda yeye mwenyewe anakua amejiandaa kwaajili yako, siku hiyo hatatoka kabisa, na hata kama ni kutoka atatoka na wewe kwakua upo, ataahirisha kutoa na marafiki.

Lakini akishakuoa kwanza utakua naye kila siku, hawezi kukiaa tena nyumbani aistoke milele kwani kashazoea, lakini hawezi kutoka na wewe kila siku kwani hajazoea kutoka na wewe na hataenjoy kila siku kutoka na wewe. Ataona kutoka na wewe kil asiku ni sawa na kuhamishia mazingira ya nyumbani Baa atakuacha nyumbani na atachelewa kurudi kama kawaida yake.

Lakini mwanamke ambaye hupenda kulalamika mara kwa mara mkiwa kwenye uchumba ukachelewa kiodgo hatalalamika kwakua itakua ni mara moja tu, ila mkishaoana ukichelewa kila siku basi atalalamika kwani atakereka. Nadhani hapa umenipata kwamba kuna mambo mengi ambayo watu huficha kwakua hawaishi pamoja, kwakua wanatumia muda mfupi pamoja tofauti na ndoa ambapo ni kila siku wanakua pamoja.

Katika Kitabu changu nimelizungumzia hili, mabadiliko haya katika ndoa ni ya lazima kwani yanaitwa kujuana, kiuhalisia unamjua mpenzi wako mume au mke vizuri miezi mitatu ya kwanza ya ndoa yenu. Kwamba huu ndiyo wakati ambao atashindwa kuficha na kujikuta anaonyesha tabia zake zote mbaya. Lakini kama ni msiri sana basi subiri miezi tisa hapa atakua hana namna.

Ila kama ni msiri zaidi basi kipindi cha kupata mtoto wa kwanza kitaonyesha rangi yake kamili hasa kwa mwanaume atabaidilika tu kama ni wa kubaidlika na asipobadilika kipindi hicho basi jua kuwa alikua haigizi ndiyo tabia zake. Sasa hapa swali kubwa ni je utafanya nini ili kumfanya mume/mke wako aisibadilike abaki kama alivyokua awali?

Mimi nadhani hapa swali kubwa si namna ya kumfanya asibadilike bali namna ya kumfanya abadilike, kwamba tabia mbaya ambazo atakuonyesha wakati wa ndoa ndiyo tabia zake na zile za wakati wa uchumba alikua anaigiza hivyo unatakiwa kumbadilisha kutoka zile za wakati wa ndoa kuja zile za uchumba. Si kazi ndogo kwani ni tabia zake za tangu utotoni hivyo unatakiwa kuwa makini hasa kwa wanaume ili asidhani kuwa unamkalia.

Hakuna kitu ambacho wanaume hawapendi kama kukaliwa na wake zao na wewe kutaka kumbadilisha ni kama kumkalia (kumpangia kila kitu), ukilalamika ni kumkalia, ukisema kwa ndugu ni kumkalia, ukihoji ni kumkalia hivyo kama unataka ndoa yako iimarike ni lazima kucheza na akili yake, nirahisi kumbaidlisha mwanaume kwa kucheza na akili yake kuliko kulalamika kila wakati!

Kuna mambo mengi ambayo nimeyazungumzia katika Kitabu changu sehemu ya pili, kama unacho hembu anza kuyasoma, ukiyatumia vizuri yale mambo basi ni rahisi sana kucheza na akili za mwanaume. Labda kwa wewe ambaye bado hujanunua Kitabu nikugusie kidogo mambo ya kufanya, kwanza kwa mwanamke unatakiwa kujua kuwa wewe ndiyo uliyeolewa, acha kushindana na maisha yake ya nyuma.

Pili ni lazima ujifunze kukataa vitu ambavyo huvipendi, najua wakati huu bado hamjazoeana hivyo unasema uchukulie poa baadhi ya mambo, useme ndiyo upya labda ataacha hapana, anza kukataa na kuonyesha kukasirika kidogo kama ukiona anafanya kitu ambacho kinakukera. Tatu hakikisha unatengeneza tamaduni zenu mpya, unamfanya ajifunze vitu vipya.

Lakini nne badilisha tabia kama vile kuchelewa kurudi nyumbani, kupenda kutokatoka na marafiki, kutokua karibu nawe kwa kutengeneza tamaduni, kwamba badala ya wewe kulalamika anachelwa kurudi hembu anza kutengeneza tamaduni ya kula chakula mapema ili awahi, lakini pia tengeneza majukumu madogo madogo ya kumfanya kua mtu mpya.

Mfundishe namna ya kukupenda, hiki kipengele utakipata sehemu ya tatu ya Kitabu changu. Nadhani hapa ndiyo unambadilisha zaidi mwanaume, badala ya kubishana naye kila kitu, kutaka kushindana hembu jishushe kidogo, si uwe mjinga hapana bali ucheze na akili yake. Soma vizuri shemu hii na jifunze mbinu mbalimbali.

Kama hujaingia kwenye ndoa au ukokatika mahusiano basi chukua fursa hii kujifunza namna ya kufanya ndoa yako isianze kwa malalamiko.



KWANINI MPENZI HUBADILIKA BAADA YA NDOA JE KUNA NAMNA YA KUMZUIA ASIBADILIKE KWANINI MPENZI HUBADILIKA BAADA YA NDOA JE KUNA NAMNA YA KUMZUIA ASIBADILIKE Reviewed by Unknown on December 28, 2017 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.